AFRIKA
2 dk kusoma
Uganda yasisitiza itapokea wahamiaji wa Marekani
Uganda imesema mpango huu ni wa muda na kwamba haitakubali kupokea watu walio na historia ya uhalifu na watoto ambao hawajaandamana na wazazi wao hawatakubaliwa.
Uganda yasisitiza itapokea wahamiaji wa Marekani
Uganda imesema iko tayari kupokea walioahamishwa kwa lazima kutoka Marekani/ picha: Reuters
4 Septemba 2025

Mwanasheria Mkuu wa Uganda anasisitiza kuwa nchi hiyo imejitolea kwa makubaliano na Marekani kupokea watu waliofukuzwa kutoka nchi hiyo.

Hayo yamethibitishwa Agosti, 2025.Hata hivyo, Uganda inasema makubaliano hayo yana masharti.

Kwa mfano Uganda imesema mpango huu ni wa muda na kwamba haitakubali kupokea watu walio na historia ya uhalifu na watoto ambao hawajaandamana na wazazi wao hawatakubaliwa.

Uganda pia imependekeza kupokea watu kutoka nchi za Kiafrika.Lakini ni lipo lengo la Uganda la kukubali makubaliano hayo?

Uganda sasa inakuwa nchi ya nne kuwapokea wananchi waliofukuzwa Marekani baada ya Rwanda, Sudan Kusini na Eswatini.

Nchi nyingine, ikiwa ni pamoja na Eswatini, zimeripotiwa kukubali mpango huo ili kuondolewa ushuru iliyowekewa na Marekani.

Nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika ambayo inauza nguo, matunda, karanga na sukari mbichi kwenda Marekani ilipigwa ushuru wa asilimia 10 na Marekani.

Mpaka kusikia mwezi Julai mwaka huu, tayari ilikuwa imepotea watu watano.Rwanda nayo imethibitisha kuwa itachukua watu 250 ingawa tarehe rasmi haijatajwa.

Wabunge nchini Uganda wamekosoa uamuzi wa nchi yao huku wakisema kuwa serikali haijapata idhini ya bunge.

Baadhi ya wananchi pia wamedai kuwa tayari nchi hiyo inakabiliwa na idadi kubwa ya wakimbizi na huenda haina uwezo wa kuchukua zaidi.

Kwa sasa, Uganda inahifadhi takriban wakimbizi milioni 2 hasa kutoka nchi jirani za DRC, Sudan Kusini na Sudan.

Huenda Uganda nayo, ikawa inatafuta afueni ya kodi kutoka kwa Marekani baada ya kutozwa ushuru wa asilimia 15 kwa bidhaa zake zitakazoingia Marekani, kama sehemu ya vita vya Trump vya kulipiana ushuru, jambo ambalo linavuruga mapato ya Uganda ya mauzo ya nje.

Mnamo mwaka wa 2024 Marekani iliiondoa Uganda katika mpango wa biashara maarufu AGOA, mkataba wa kibiashara ambao ulichangia pakubwa katika mauzo ya Uganda nchini Marekani.

Hii ilikuwa baada ya serikali kupitisha Sheria ya Kupinga Mapenzi ya Jinsia Moja.

Baadhi ya wananchi wa Uganda wameonyesha wasiwasi wao wa nchi hiyo kupokea watu ambao wanaweza kuwa na rekodi za uhalifu.

Nchi hizo mbili bado hazijafafanua ni mkakati gani utakaotumika kutekeleza makubaliano hayo.

CHANZO:TRT Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us