tokea masaa 18
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) siku ya Jumanne, itasikiliza kesi ya kihistoria dhidi ya Joseph Kony, kiongozi wa kundi la waasi la Lord’s Resistance Army (LRA), ambaye amekuwa mafichoni kwa zaidi ya miaka 30.
Kony anakabiliwa na mashitaka 39 ya uhalifu wa kivita na dhidi ya ubinadamu, yakiwemo mauaji, ubakaji, utumwa wa kingono, na utekaji wa watoto.
Zilizopendekezwa
Kesi hiyo inasikilizwa bila uwepo wake mahakamani hapo, mara ya kwanza katika historia ya mahakama hiyo, kwa lengo la kuthibitisha ushahidi wa kutosha ili kuendelea na hatua za kisheria, hata bila uwepo wa mtuhumiwa.
Kony, ambaye alianzisha LRA katika miaka ya 1980 akidai kuunda taifa linaloongozwa na Amri Kumi za Biblia, anasadikiwa kujificha katika misitu ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.