AFRIKA
2 dk kusoma
Zaidi ya miili 370 yapatikana baada ya maporomoko ya ardhi eneo la Darfur, Sudan
Zaidi ya watu 1,000 wamefariki katika kijiji kimoja eneo la Kati la Jimbo la Darfur baada ya maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa
Zaidi ya miili 370 yapatikana baada ya maporomoko ya ardhi eneo la Darfur, Sudan
tokea masaa 9

Miili zaidi ya 370 imepatikana baada ya maporomoko mabaya ya ardhi yalisababisha vifo vya karibu watu 1,000 Darfur magharibi mwa Sudan, kundi moja la Sudan lilisema siku ya Alhamisi.

Ibrahim Hasbullah, afisa wa Sudan Liberation Movement (SLM), anasema wamefanikiwa kupata miili zaidi ya 370 kutoka kwenye kifusi katika kijiji cha Tarsin eneo la Kati la Jimbo la Darfur.

“Kwa wale wengine waliofariki, hatukuweza kutoa miili yao kwa kuwa ilikuwa iko chini ya miamba ilhali wengine walisombwa na mabonde,” aliongeza katika video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Katika taarifa siku ya Alhamisi, SLM ilisema kijiji hicho kilokumbwa na mkasa “kiko katikati ya Jebel Marra, mchanga wa volkano ambao hauwezi kuhimili maporomoko pindi kunapokuwa na mvua kubwa.”

Kulingana na vyanzo vya eneo hilo, watu zaidi ya 1,000 waliuawa siku ya Jumanne katika kijiji hicho kutokana na maporomoko yaliyosababishwa na mvua kubwa.

SLM ni moja ya kundi kubwa la wapiganaji eneo la Darfur ambalo limekuwa likipigana dhidi ya serikali tangu 2003. Tofauti na makundi mengine ya wapiganaji, wamekataa mpango wa amani na serikali ya Sudan.

Kundi hilo linadhibiti baadhi ya maeneo ya Darfur ya Kati, ambayo pia yanadhibitiwa na wapiganaji wa Rapid Support Forces (RSF).

Siku ya Jumanne, Baraza la serikali ya Sudan lilisema linajitahidi kukusanya wanachoweza kwa ajili ya kuwasaidia wale walioathirika huko Tarsin.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us