AFRIKA
2 dk kusoma
DRC yatangaza mlipuko mwingine wa Ebola, watu 15 wafariki
Maambukizi 28 yameripotiwa katika mkoa wa Kasai, huku vifo vikiwa asilima 57 vilivyothibitishwa na taasisi ya utafiti ya kitaifa, amesema Waziri wa Afya Roger Kamba
DRC yatangaza mlipuko mwingine wa Ebola, watu 15 wafariki
tokea masaa 11

Mlipuko wa Ebola umesababisha vifo vya watu 15, ikiwemo wafanyakazi wanne wa afya, katika eneo la Mweka mkoa wa kusini wa Kasai, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, waziri wa afya alitangaza Alhamisi, ikiwa ni mlipuko wa 16 wa virusi hivyo katika kipindi cha miongo mitano iliopita.

"Kwa niaba ya Wizara ya Afya, Natangaza rasmi kuzuka tena kwa ugonjwa wa Ebola, ule aina ya Zaire, katika eneo la Boulape, Mkoa wa Kasai," Waziri wa Afya Roger Kamba aliwaambia waandishi wa habari.

Kamba alisema maambukizi 28 yameripotiwa kufikia sasa, huku asilimia 57 ya vifo vikithibitishwa na taasisi ya utafiti ya kitaifa.

Takwimu hizi ni za muda huku uchunguzi ukiendelea, lakini matokeo zaidi yanatarajiwa hivi karibuni, aliongeza.

Waziri huyo alisema serikali imeanzisha vituo vya dharura kushughulikia hilo.

Maafisa wamepelekwa katika maeneo hayo, na tathmini imeimarishwa, na utaratibu wa kuwatenga wanaoonekana kuwa na dalili umeanzishwa, pamoja na namna watu wanaweza kufanya mazishi ili kulinda jamii, waziri amesema.

DRC imekabiliwa na milipuko kadhaa ya Ebola, huku maambukizi yakiripotiwa eneo la Kivu Kaskazini mwaka 2022 na 2023, kusababisha vifo vingi.

Virusi vya Ebola vimekuwepo katika taifa hilo la Afrika ya Kati, ambapo mlipuko huu wa sasa ni wa 16 tangu 1976.

Milipuko ya Ebola aina ya Zaire imetokea mara kadhaa, lakini nchi imekabiliana nayo kupitia juhudi za kufuatilia kwa karibu, kutibu, na chanjo, kama vile mpango wa chanjo ya rVSV-ZEBOV na uthibitishwaji wa mtandao wa INRB.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us