AFRIKA
2 dk kusoma
Boko Haram: Mashambulizi ya angani Nigeria yawaua magaidi zaidi ya 15 katika msitu
Mashambulizi ya angani yamelenga eneo jipya la magaidi magharibi mwa Zuwa katika sehemu ya Sambisa, anasema msemaji wa Jeshi la Anga la Nigeria
Boko Haram: Mashambulizi ya angani Nigeria yawaua magaidi zaidi ya 15 katika msitu
Operesheni hiyo iliwalenga wapiganaji na makamanda waliohusika na mashambulizi ya hivi karibuni. / REUTERS
tokea masaa 14

Jeshi la Anga la Nigeria (NAF) limewaua zaidi ya magaidi 15 wa Boko Haram huko Zuwa, Msitu wa Sambisa, Kaskazini mashariki mwa Nigeria, afisa mmoja alisema Alhamisi.

NAF imewaua magaidi wa Boko Haram zaidi ya 15 siku ya Jumatano kama sehemu ya Kikosi Kazi cha pamoja cha operesheni Hadin Kai cha Kaskazini Mashariki, kulingana na taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Anga, Ehimen Ejodame.

Aliongeza kuwa mashambulizi ya anga yanadhihirisha uhakika wa NAF, katika mapambano dhidi ya ugaidi.

“Septemba 3 2025, mpango wa uhakika ulipangwa na kutekelezwa kwa kushambulia eneo jipya la magaidi magharibi mwa Zuwa katika sehemu ya Sambisa.”

‘Maeneo muhimu yameharibiwa’

“Kupitia taarifa mahsusi za kijasusi na uchunguzi thabiti, tumelenga maeneo ya wapiganaji ya kujificha na makamanda wanaohusika na ukatili wa hivi karibuni katika eneo la Bitta.”

“Mashambulizi hayo yamewaumiza sana, na kuwakata makali zaidi ya magaidi 15 wa Boko Haram na kuharibu maeneo yao muhimu kwa ajili ya operesheni zao,” kulingana na taarifa hiyo.

Mafanikio haya ya hivi karibuni yanadhihirisha uthabiti wa jeshi la anga kulinda maisha na mali za watu wa Nigeria huku likitoa msaada kwa vikosi vya ardhini katika operesheni ya pamoja kwa lengo la kusambaratisha mtandao wa magaidi, ilisema.

“Jeshi la Anga la Nigeria linaendelea kuwa ishara ya ukakamavu, utaalamu, na umakini katika kutumia uwezo wa anga kwa lengo la kulinda usalama wa taifa,” taarifa hiyo ilisema.

Boko Haram ni kundi la kigaidi lenye makao yake kaskazini mashariki mwa Nigeria, ambalo pia liko Chad, Niger, na Cameroon. Kundi hilo linajulikana kwa mashambulizi ya kikatili dhidi ya raia, vikosi vya ulinzi na usalama, na taasisi za elimu, ikiwemo kufyatulia watu risasi, mashambulizi ya mabomu, na utekaji nyara.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us