Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) nchini Tanzania kimewaomba Watanzania kukipa ridhaa ya kuiongoza nchi hiyo, kwa ahadi ya kusukuma mbele vuguvugu la mabadiliko katika nchi hiyo.
Akizungumza mjini Morogoro, mgombea mwenza wa urais wa chama hicho, Devotha Minja amesema ni vyema watanzania wakakichagua chama hicho, ili kiharakishe ajenda ya mabadiliko na mageuzi.
Kulingana na Minja, wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanapaswa kukichagua CHAUMMA iki ikabili mifumo ya kodi ambayo si rafiki kwa wananchi.
“Kama CHADEMA hawapo, basi mtuunge mkono mkono kwa sababu adui yetu ni CCM, tunazitaka ‘reforms’…tukiingia bungeni itakuwa ni reforms, reforms, reforms. Hicho ndicho kitakachokuwa kipaumbele cha CHAUMMA,” alisema Minja.
Minja alisisitiza kuwa ni ngumu kupata mabadiliko unayoyataka kama hauna wawakilishi bungeni wa kuleta mabadiliko hayo.
Mgombea huyo ameongeza kuwa chama chake kimejizatiti kuboresha sekta ya kilimo ili kiwe na tija kwa wakulima nchini Tanzania.