AFRIKA
4 dk kusoma
Hospitali ya Recep Tayyip Erdoğan: Daraja la afya na undugu nchini Somalia
Hospitali hii pia imekuwa daraja katika safari ya Somalia kuelekea ustawi wa kudumu, ikipiga jeki ufufuaji wa mfumo dhaifu wa afya uliodorora kwa miongo kadhaa kutokana na vita vya ndani na miundombinu dhaifu na isiyotosha.
Hospitali ya Recep Tayyip Erdoğan: Daraja la afya na undugu nchini Somalia
Ujenzi wa Hospitali hii ni ishara ya urafiki na udugu kati ya nchi hizo mbili. / TRT Afrika Swahili
tokea masaa 17

Tangu ilipoanzishwa mwaka wa 2015 katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, pindi ujenzi wake ulioanza mwaka 2012 ulipokamilika, Hospitali ya mafunzo na utafiti ya Recep Tayyip Erdoğan, iliyopewa jina la Rais wa Uturuki, imekuwa kivutio cha raia wa Somalia.

Hii leo, hospitali hiyo inatoa huduma za matibabu kwa takriban wagonjwa 40,000 kila mwezi wanaotoka sehemu mbalimbali ikiwemo ndani ya Somalia na hata kutoka mataifa jirani kama Kenya, Uganda na Ethiopia.

Ikiwa mojawapo ya hospitali kubwa zaidi nchini Somalia, moja ya vituo vikuu vya afya Afrika Mashariki, na mradi mkubwa zaidi wa kibinadamu wa afya nje ya Uturuki, Hospitali ya Recep Tayyip Erdoğan imetambulika kama ishara inayoonekana zaidi ya udugu kati ya Uturuki na Somalia.

Kwa Wasomali, ni zaidi ya hospitali, na chemchemi ya imani na matumaini.

Ikiwa na uwezo wa vitanda takribani 250, hospitali imejengwa kwa vifaa vya kisasa vinavyojumuisha huduma za dharura, wagonjwa mahututi, vyumba nane za upasuaji, vitengo vya uzazi, kitengo cha kutibu majeraha ya moto, kitengo cha kusafisha damu (dialysis), na idara ya uchunguzi wa mishipa ya damu (angiography).

Hospitali hii pia imekuwa daraja katika safari ya Somalia kuelekea ustawi wa kudumu, ikipiga jeki ufufuaji wa mfumo dhaifu wa afya uliodorora kwa miongo kadhaa kutokana na vita vya ndani na miundombinu dhaifu na isiyotosha.

Daktari Mkuu, Dr. Ibrahim Agaoglu, amesisitiza kuwa lengo la hospitali sio la kibiashara. “Madhumuni halisi ya hospitali hii ni kutoa huduma za afya za kiwango cha juu bila gharama au kwa gharama nafuu zaidi kwa wanaohitaji.

Hospitali hii inatoa huduma bora na za kipekee katika nyanja nyingi nchini.”Ameongeza: “Kwa msaada wa Rais wetu, hospitali hii siyo tu kituo cha huduma za afya, bali pia inawakilisha udugu kati ya watu wa Somalia na Uturuki. Hili ni wazi katika kila nyanja - kuanzia usimamizi hadi wafanyakazi wote. Tunatoa huduma kupitia juhudi za pamoja za wafanyakazi wa Kisomali na Kituruki. Kwa sasa, tunao madaktari wa Kisomali wapatao 170, madaktari wa Kituruki wapatao 30, jumla ya wafanyakazi wa Kisomali 1,040 na wafanyakazi wa Kituruki 80.”Hospitali pia limesifika kwa mchango wake wa utoaji wa elimu ya afya.

Kila mwaka, mamia ya madaktari, wauguzi na wahudumu wa afya wa Kisomali hupokea mafunzo na uzoefu wa vitendo pamoja na wataalamu kutoka Uturuki. Hili ni jambo la kimkakati katika kusaidia Somalia kukuza nguvu kazi yake ya kitabibu, kama alivyofafanua Daktari Agaoglu.“Hospitali yetu ndio hospitali ya pekee ya kigeni ambapo taifa moja linawafundisha madaktari wa taifa jingine.

Sio madaktari bora pekee, katika eneo hili hili kuna Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya ambapo pia tunaandaa wauguzi na mafundi wa tiba. Kwa mfano, madaktari wawili pekee wa upasuaji wa kifua nchini ni wahitimu wa hospitali hii na sasa wanafanya kazi hapa. Wataalamu tunaowaandaa huajiriwa hapa na katika hospitali nyengine nchini Somalia kulingana na mahitaji ya serikali.

Huduma nyingi za afya na shughuli za kielimu hapa zinaendeshwa na wafanyakazi wa Kisomali tuliowaandaa, huku wataalamu kutoka Uturuki wakifanya uratibu, usimamizi na kujaza mapengo pale panapohitajika.

”Hospitali ya Recep Tayyip Erdoğan pia imekuwa kituo muhimu wakati wa majanga na milipuko ya maradhi. Wakati wa janga la Uviko-19, maelfu ya vipimo na matibabu yalifanyika hapa.”

Agaoglu aliongeza kuwa mbali na huduma za afya, hospitali pia inaendesha programu za elimu.

“Tangu mwaka 2020, tumewafunza madaktari bingwa 128 ambao sasa wanahudumu katika hospitali yetu au katika vituo vyengine nchini Somalia. Hapo awali, kutokana na ukosefu wa wataalamu, maafa yalitokea hata kutokana na maradhi yanayoweza kutibika virahisi.

Sasa watu hawalazimiki tena kusafiri nje ya nchi kutafuta tiba.”Naibu Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Muhammed Hussein Ashraf, alielezea kuwa hospitali hii kama “mfano hai wa diplomasia ya kibinadamu” na kutoa shukrani za dhati kwa serikali ya Uturuki kwa kutoa huduma kama hii kwa jamii ya Kisomali.“

Awali, watu walilazimika kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya huduma za kimatibabu, lakini sasa huduma nyingi zinapatikana hapa, na watu wanaitambua hospitali hii kama kituo bora cha afya.Tunapokea pongezi nyingi kutoka kwa jamii.

Pia tunawasaidia wagonjwa maskini na wanyonge wasioweza kugharamia matibabu. Huduma kama vile kituo cha kutibu majeraha ya moto na vyumba vya wagonjwa mahututi, ambazo hazipatikani katika hospitali za binafsi nchini Somalia, zinatolewa bure kwa wale wasioweza kumudu.”

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us