AFRIKA
2 dk kusoma
Rais wa Uganda afanya ziara Misri, maongezi kuhusu mto Nile yatarajiwa kufanyika
Ziara yake ni ya kidiplomasia inayolenga kuimarisha uhusiano wa pande mbili na kuendeleza ushirikiano wa kikanda kwenye Mto Nile.
Rais wa Uganda afanya ziara Misri, maongezi kuhusu mto Nile yatarajiwa kufanyika
Rais wa Uganda Yoweri Museveni yuko Misri kwa ziara ya siku tatu/ picha Rais Yoweri Museveni / Public domain
tokea masaa 6

Rais wa Uganda Yoweri Museveni yupo jijini Cairo nchini Misri tangu Agosti 11, 2025, katika ziara rasmi ya siku tatu kwa mwaliko wa Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi.

“Nimefika katika nchi yetu ya kindugu ya Misri kwa mwaliko wa Mheshimiwa Abdel Fattah el-Sisi. Ninatazamia kushirikiana naye juu ya njia za kukuza uhusiano wetu wa nchi mbili,” Rais Museveni alisema katika taarifa mtandaoni.

Ziara yake ni ya kidiplomasia ikilenga kuimarisha uhusiano wa pande mbili na kuendeleza ushirikiano wa kikanda kwenye Mto Nile.

Misri na Uganda zina Mto Nile ambao Misri unauangalia kama msingi wa uhai wake.

Ziara hiyo inajiri chini ya wiki moja baada ya Museveni kuwa mwenyeji wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Dkt. Badr Abdellaty, katika Ikulu ya Entebbe kwa majadiliano ya ngazi ya juu kuhusu maendeleo ya Mto Nile.

Wakati na mazungumzo Entebbe, Museveni alisema changamoto kubwa zaidi ya Mto huo sio migogoro ya kijiografia, lakini uharibifu wa mazingira na maendeleo duni katika nchi zinazopakana na mto.

Alitaja ukataji miti unaosababishwa na jamii kukosa umeme na "kilimo cha zamani" kama hatari kubwa kwa afya ya muda mrefu.

"Nchi zote wadau wa Nile lazima zishiriki katika mijadala ya juu kuhusu jinsi bora ya kutumia Mto Nile bila kuhatarisha uwepo wake," Museveni alisema.

Ziara ya Rais Museveni inatarajiwa kuendeleza mijadala hiyo, huku usimamizi wa rasilimali za maji, ustahimilivu wa hali ya hewa, na maendeleo ya miundombinu.

Uganda katika siku za nyuma imeelezea utayari wake wa "kusaidia kukuza mazungumzo kati ya mataifa yote ya Bonde la Mto Nile ili kuepuka migogoro na kuhakikisha ugawaji wa faida sawa," iliongeza ripoti hiyo.

Misri na Ethiopia bado zina mvutano kuhusu matumizi ya maji ya Mto Nile, huku Misri ikipinga ujenzi wa bwana unaofanywa na Ethiopia katika Mto huo huku Ethiopia ikijiteteta kuwa ina haki ya kutumia rasilimali hiyo kwa maendeleo ya wananchi wake.

CHANZO:TRT Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us