Kampuni ya nguo ya ZARA Uingereza matatani kwa kutumia mamodo 'wembamba kupita kiasi'
Kampuni ya nguo ya ZARA Uingereza matatani kwa kutumia mamodo 'wembamba kupita kiasi'
Kampuni hiyo ya kuuza nguo za mitindo imelazimishwa kuondoa picha za mauzo mtandaoni kutokana na mamodo waliotumiwa wanaohofiwa kuwa wasio na afya njema kutokana na wembamba wao
11 Agosti 2025

ZARA imejikuta katika mzozo na mamlaka ya kudhibiti viwango vya matangazo ya mauzo ya Uingereza (ASA) baada ya mamlaka hiyo kuilazimisha ZARA kuondoa picha za matangazo ya biashara walizochapisha mtandaoni kutokana na hofu ya afya ya mamodo waliotumika.

ASA imelalamika kuwa mamodo hao wamedhoofika kupita kiasi huku ikiangazia mifupa iliyojitokeza wazi shingoni miguuni na mgongoni.

Mamlaka hiyo imesema kuwa huo ni ukiukaji wa masharti ya matangazo ya umma.

ZARA imeshutumiwa kuendekeza mtindo mbaya wa maisha ulio hatari kwa afya ya watazamaji hasa vijana na watoto.

Mamodo walitumika kwengine

‘Kwa ujumla tunazingatia kuwa mkao wa modo na chaguo la mavazi kwenye tangazo ziliunda hisia kwamba modo huyo alikuwa mwembamba kupita viwango vya afya.’’ ASA ilisema.

Kutokana na hilo, ZARA ililazimika kuondoa picha nne kati ya zile walizokuwa wamechapisha.

‘‘Kulingana na vigezo vya ASA, mamodo hao walikuwa wametoa shahada za uthibitisho wa afya, kuendana na azimio la kuimarisha afya njema katika fesheni,’’ iliandika ZARA.

Kampuni hiyo ilisisitiza kuwa mamodo hao wametumika katika matangazo mengine mengi ya mitindo na walithibitishwa kuwa na afya nzuri.

Hii sio mara ya kwanza

Sheria ya Uingereza inasema ni lazima mamodo wote wanaotumika waonyeshe shahada za afya kutoka kwa madaktari wenye utaalamu wa kutambua matatizo ya kula na afya.

Mnamo Desemba 2023, ZARA iliendesha kampeni ya tangazo iliyopewa jina la "Jacket," inayoonyesha misanamu iliyofunikwa kwa sanda nyeupe karibu na majengo yaliyobomoka na kusababisha shutuma kali kutoka kwa umma.

ZARA iliiondoa tangazo hilo na kutoa msamaha usio wa kuwajibika bila kuzungumzia uhusiano wake na Israel.

Kampuni ya nguo ya Uingereza ya Marks & Spencer pia iliwahi kulazimishwa kuondoa tangazo lake na ASA mwaka 2023 kwa shutuma la kutumia modo aliyeonekana "mwembamba kupita kiasi."

Mamlaka ya Viwango vya Utangazaji (ASA) ilihitimisha kuwa "haikuwajibika" kwa muuzaji rejareja kutumia picha hiyo kutangaza nguo kwenye programu yake ya simu.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us