AFRIKA
1 dk kusoma
Kenya wawanolea makucha Morocco katika mkutano wa kwanza wa Kundi A katika uwanja wa Kasarani
Kenya wawanolea makucha Morocco katika mkutano wa kwanza wa Kundi A katika uwanja wa Kasarani
Kenya yajiandaa kwa mechi yao ngumu zaidi ya makundi dhidi ya Morocco / CAF
10 Agosti 2025

Kenya na Morocco zinakutana kwa mara ya kwanza katika michuano ya TotalEnergies CAF ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) zitakapochuana katika Kundi A katika Uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Moi, Nairobi, Jumapili.

Morocco, ambayo haijafungwa katika mechi tano zilizopita na timu pinzani za Afrika Mashariki (ushindi tatu, sare mbili), ina rekodi kubwa katika mechi kama hizo. Waliifunga Uganda mara mbili 2014 na 2020, wakashinda 4-1 dhidi ya Rwanda 2016, na walitoka sare ya 0-0 na Sudan 2018 na Rwanda 2020. Michezo yote hii ilikuwa katika hatua ya makundi.

Kenya ambayo ni mara ya Kwanza wanashiriki mashindano haya ya CHAN, wameponea Bila kufungwa baada ya mechi mbili: waliifunga DR Congo 1-0 na wakatoka sare ya 0-0 na Angola.

kwa upande mwingine Palancas Negras ya Angola na Chipolopolo ya Zambia wanajikuta katika mapambano ya hali ya juu ambayo yataweka wazi kampeni zao za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika ya TotalEnergies (CHAN) 2024.

Kwa Angola, jambo ni moja - piga ua lazima washinde la sivyo waanze kujiandaa kuyaaga mashindano haya. Kwa Zambia, ni nafasi ya kufufua matumaini yao na kuweka ndoto yao hai.


CHANZO:CAF
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us