AFRIKA
2 dk kusoma
Reli ya SGR Tanzania kuanza kubeba mizigo
Mabehewa hayo yalifanyiwa majaribio ikiwa ni pamoja na tathmini za nguvu ili kuhakikisha uimara na utendaji wake.
Reli ya SGR Tanzania kuanza kubeba mizigo
Reli ya SGR ya abiria tayari imeanza kutoa huduma/ Picha: Reuters
4 Juni 2025

Shirika la Reli Tanzania (TRC) linatarajia kuanza shughuli zake za kibiashara za usafirishaji wa mizigo kwa Reli ya Standard Gauge (SGR) baada ya kufanyiwa majaribio kwa mafanikio.

Treni ya mizigo yenye urefu wa kilomita mbili inayofanya kazi kati ya Dar es Salaam na Dodoma inatarajiwa kuongeza kwa kiasi kikubwa ufanisi wa vifaa na kufungua fursa mpya za biashara nchini kote.

"Tumekamilisha upimaji unaohitajika na kupata cheti kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA), hivyo tuko tayari kuanza shughuli za usafirishaji wa mizigo," Mhandisi Enock Mgonja, Meneja wa Utunzaji wa Mabehewa ya Abiria na Mizigo wa TRC, alisema.

Aliongeza kuwa mabehewa hayo yalifanyiwa majaribio chini ya usimamizi wa LATRA, ikiwa ni pamoja na tathmini za nguvu, ili kuhakikisha uimara na utendaji wao.

Afisa Usafirishaji Mwandamizi wa TRC, Masha Yasin, alisema kuwa kituo kikuu cha reli ya mizigo ni bandari ya Dar es Salaam.

Alibainisha kuwa vituo vya mabehewa ya kubebea mizigo vimeainishwa, huku vyengine vikiwa maalum kwa huduma za abiria na vyengine kwa usafirishaji.

"Tuna vituo kama Ruvu, Pugu, Morogoro, na Ihumwa, ambavyo vitatumika kwa treni ya mizigo," alisema tarehe rasmi ya shughuli zote za kibiashara itatangazwa kwa wakati ufaao.

Mnamo Disemba 2024, TRC ilipokea mabehewa 264 kutoka China, ambayo yalikuwa sehemu ya agizo kubwa ya 1,430.

Shehena hiyo ilijumuisha mabehewa 200 za kontena na mabehewa 64 yaliyoundwa mahsusi kubeba mizigo mingine.


CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us