Kaka yake mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Ureno Andre Silva pia alifariki katika ajali hiyo, ambayo ilitokea mkoa wa Hispania wa Zamora.
Andre Silva mwenye umri wa miaka 26 pia alikuwa mchezaji wa kulipwa, na klabu ya daraja la pili ya nchini Ureno Penafiel.
Polisi nchini Hispania wanasema kuwa Jota na kaka yake walifariki usiku wa kuamkia Alhamisi.
Walisema kuwa gari yao, aina ya Lamborghini, ilipasuka tairi wakati wakipita gari lingine na kuteketea.
Jota alimuoa mwenza wake wa muda mrefu Rute Cardoso, mwezi uliopita ambaye tayari alikuwa amepata naye watoto watatu.
Ni hivi majuzi tu ambapo aliweka picha za sherehe hizo zilizofanyika 22 Juni kwenye mitandao ya kijamii.
Jota alisaidia Liverpool kushinda taji la Ligi Kuu ya England msimu uliopita na pia akacheza kwenye mashindano ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya ambapo Ureno iliishinda Hispania katika fainali mwezi Juni.