AFRIKA
2 dk kusoma
Mzize 'Goal Machine': Mshambulizi mwenye ari kubwa aliyelenga macho kwa ubingwa wa CHAN
Kwa Tanzania, ulikuwa ni zaidi ya ushindi—ulikuwa ushindi wa tatu mfululizo wa hatua ya makundi na tikiti ya kihistoria ya kutinga hatua ya robo fainali ya Mashindano ya TotalEnergies African Nations Championship (CHAN) 2024.
Mzize 'Goal Machine': Mshambulizi mwenye ari kubwa aliyelenga macho kwa ubingwa wa CHAN
Huku robo fainali sasa ikithibitishwa, Suleiman alielekeza mawazo yake kwa wafuasi wa Tanzania./ CAF
tokea siku moja

Tangu kulia kipenga cha kuanza mechi, uwanja ulitetema kwa kishindo cha Clement Francis Mzize.

Mshambuliaji huyo alikimbia, alidodosa na alichenga, huku macho yake yakilenga kutikisa wavu wa adui.

lakini Mzize hakufunga tu - aliunguruma, na kutoa mabao mawili ndani ya dakika 20 na kuizamisha Madagascar na kuupeleka Uwanja wa Benjamin Mkapa kupasuka kwa sauti za mashabiki waliojawa furaha tele. Kwa mashabiki wa Madagascar, iwapo hawakujua, hiyo tayari ilikuwa dalili kuwa Tanzania ni moto wa kuotea mbali.

Hadi kufikia mwisho wa usiku, ubao wa matokeo ulisomeka 2-1 kwa wenyeji, na Mzize alikuwa ametawazwa kuwa mchezaji bora wa mechi wa TotalEnergies.

Zaidi ya Ushindi

"Namshukuru Mungu kwa nafasi hii ya kuwa katika nafasi hii na kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi,’’ alisema Mzize. ‘‘Ni vyema tukaendelea kusonga mbele katika mashindano hayo, na tunatumai kufika mbali katika michuano ya Mataifa ya Afrika ya TotalEnergies 2024." Aliwaambia waandishi wa habari baada ya mechi.

Kwa Tanzania, ulikuwa ni zaidi ya ushindi—ulikuwa ushindi wa tatu mfululizo wa hatua ya makundi na tikiti ya kihistoria ya kutinga hatua ya mtoano ya Mashindano ya TotalEnergies African Nations Championship (CHAN) 2024.

Kwa taifa linalopenda soka lakini bado linafuatilia mafanikio makubwa ya bara, wakati huu waliandika historia.

Kutokana na ujasiri wake na utulivu mbele ya lango, Clement Francis Mzize ameibuka kuwa mmoja wa wachezaji wanaotazamwa zaidi CHAN 2024.

Wachezaji walijitolea

Katika mkutano wake na waandishi wa habari baada ya mechi, Kocha Hemed Suleiman alihakikisha kuwa mwangaza unawaangazia wachezaji wake.

"Nawaambia wachezaji, mmefanya vizuri. Si rahisi kushinda mechi tatu kwenye michuano hiyo. Ilikuwa ni mechi ngumu, na wachezaji wetu walifanya kazi nzuri. Tulijaribu kuishinikiza Madagascar tangu mwanzo. Kulikuwa na nyakati ngumu wakati wa mchezo kwa ujumla."

Aliongeza: "Tunaamini tulitimiza kile tulichohitaji katika mechi hiyo. Wachezaji walijitolea kwa muda wote, na matokeo yalikuwa ya haki."

Huku robo fainali sasa ikithibitishwa, Suleiman alielekeza mawazo yake kwa mashabiki wa Tanzania.

"Ukweli kwamba tumefuzu hatua inayofuata - lazima niwaambie Watanzania waendelee kutuunga mkono na kuwatia moyo wachezaji, na kuweka mazingira hayo. Tumefikia hatua hii pamoja kwenye mashindano."

CHANZO:CAF
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us