MICHEZO
2 dk kusoma
CHAN 2024: Kenya na DRC kumenyana leo uwanja wa Kasarani
Kenya kuonja utamu wa CHAN kwa mara ya kwanza kabisa inapokutana na washindi mara mbili DRC jijini Nairobi
CHAN 2024: Kenya na DRC  kumenyana leo uwanja wa Kasarani
Hii ni mara ya kwanza kwa Kenya kushiriki CHAN, lakini DRC imeshinda kombe mara mbili / CAF
3 Agosti 2025

Harambee Stars ya Kenya itaanza safari yake ya kihistoria katika michuano ya TotalEnergies CAF ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) PAMOJA 2024 Jumapili kwa mchuano mkali wa Kundi A dhidi ya mabingwa mara mbili DR Congo kwenye Uwanja wa Kasarani jijini Nairobi.

Huku mataifa matano yakipigania nafasi mbili pekee za robo-fainali katika Kundi A, kila mechi inakuwa na umuhimu zaidi - na wenyeji wako chini ya shinikizo la kuwasilisha matokeo kutoka kwa kipemga cha kwanza.

Ratiba hii ya ufunguzi inaashiria kurejea kwa Kenya katika hatua ya bara na inaahidi kuweka sauti kwa kile kinachotarajiwa kuwa mojawapo ya matoleo yenye ushindani mkubwa hadi sasa.

Wanaingia ugani chini ya maelekezo ya kocha mkuu Benni McCarthy.

Vigogo walihama timu

Mtaalamu huyo wa Afrika Kusini aliyeteuliwa mwezi Machi, alifanikiwa kuipatia Harambee Stars motisha na kujiamini na ustadi wa kisasa wa kimbinu, lakini maandalizi ya timu hiyo katika michuano hiyo yameathiriwa na kuondoka kwa wachezaji kusikotarajiwa na wasiwasi wa utimamu wa mwili.

Washambuliaji wakuu Moses Shumah na Emmanuel Osoro - wafungaji wawili bora wa Ligi Kuu ya FKF - awali walikuwa sehemu ya kikosi kabla ya kuhamia klabu ya Power Dynamos ya Zambia. Kijana anayechipukia, Mohamed Bajaber alifuata mfano huo, na kukamilisha uhamisho wa hali ya juu kwenda Simba SC ya Tanzania usiku wa kuamkia shindano hilo.

Mnammo Jumamosi Rais wa Kenya William Ruto pia alitilia sukari utamu wa shindano kwa Wakenya akiwaahidi kila mchezaji shilingi milioni za Kenya kwa kila mechi watakayoshinda.

Beki Pamba Swaleh yuko nje kutokana na changamoto za kiafya huku kiucgo cha kati Brian Musa akiwa na jeraha.

Hata hivyo Kocha McCarthy bado ana matumaini

"Ndio, tumekumbana na vikwazo, lakini wachezaji wameonyesha tamaa na ari kubwa. Uchaguzi wa kikosi cha kwanza umekuwa mgumu, lakini nina imani kwamba yeyote atakayeingia uwanjani ataifanya nchi kujivunia."

DRC wanakuja ‘kulipiza kisasi’

Kwa upande mwingine, DR Congo - timu iliyofanikiwa zaidi katika historia ya CHAN ikiwa na mataji mawili (2009 na 2016) - inafika ikiwa na kisasi kikubwa cha kulipiza katika shindano hili.

Leopards walipata kipigo cha kukatisha tamaa nchini Algeria miaka miwili iliyopita, wakitoka katika hatua ya makundi bila bao hata moja.

Kocha Otis Ngoma Kondi amedhamiria kurekebisha makosa hayo. "Hatuko hapa kwa ajili ya utalii," alisema kwa msisitizo. "Ni mashindano. Hali ya hapa Kenya ni nzuri, lakini tunaangazia soka kikamilifu."

Licha ya muda wa maandalizi kukatishwa na mechi moja pekee ya kirafiki kabla ya kuanza, Ngoma anaamini kikosi chake kiko tayari.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us