tokea masaa 16
Watu nane wamepoteza maisha baada ya basi dogo walilokuwa wakisafiria kugonga treni ya mizigo nchini Kenya.
Kulingana na Kamanda wa Polisi wa Naivasha, Anthony Keter ajali hiyo iliyotokea jioni ya Agosti 7, 2025, ilihusisha treni ya mizigo na basi dogo la kampuni ya Kenya Pipeline (KPC).
Kwa mujibu wa Keter, ajali hiyo imetokea katika makutano ya Morendat, Kaunti ya Nakuru.