Novatus Miroshi amezaliwa Tanzania mwaka 2002, ana umri wa miaka 22. Amewahi kucheza soka katika vilabu vya Biashara United na Azam FC nchini Tanzania. Nje ya Tanzania amepata fursa ya kuchezea timu za Maccabi Tel Aviv na Beitar Tel Aviv Bat Yam za Israel.
Pia amewahi kuwa katika klabu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine ambapo pia alipata fursa ya kucheza katika ligi ya klabu bingwa barani Ulaya. Mwaka 2022 alisaini mkataba na timu ya Zulte Waregem ya Ubelgiji.
Alijiunga na Goztepe ya Uturuki Julai mwaka 2024 na anatarajiwa kuwepo na timu hiyo hadi katikati mwa mwaka 2028.
Mwezi huu aliifungia timu yake ya Goztepe magoli mawili na kuisadia kupata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya klabu nyingine ya ligi kuu Rizespor.
Alianza kucheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa kwa timu ya Tanzania Februari 2021 ikiwa ni kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20.
Mwaka huo huo mwezi Septemba akapata fursa ya kuichezea Taifa Stars katika mechi yao dhidi ya DR Congo.
Miroshi ambaye ametajwa kama mchezaji hodari wa safu ya ulinzi amehusishwa na baadhi ya vilabu vingine kutaka huduma, ila kwa sasa anawapa burudani na uhakika mashabiki wa Goztepe, huko Izmir.