UTURUKI
1 dk kusoma
Shambulio la Israel dhidi ya Qatar linapaswa kuwa onyo kwa eneo lote
Israel "imeweka wazi tena kwamba haitambui mamlaka ya nchi yoyote," amesema Numan Kurtulmus.
Shambulio la Israel dhidi ya Qatar linapaswa kuwa onyo kwa eneo lote
Spika wa Bunge la Uturuki, amesema kuwa mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel dhidi ya nchi za ukanda huu yanapaswa kuwa "onyo". / AA
11 Septemba 2025

Spika wa Bunge la Uturuki, Numan Kurtulmus, amesema kuwa mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel dhidi ya nchi za ukanda huu yanapaswa kuwa "onyo".

Kauli hiyo ya Kurtulmus ilitolewa siku ya Alhamisi katika kikao cha Kamati ya Mshikamano wa Kitaifa, Undugu na Demokrasia, ambayo ilianzishwa katika bunge la Uturuki kama sehemu ya mchakato wa "Uturuki isiyo na ugaidi".

Akiweka wazi kuwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Qatar, Tunisia, na Yemen yanatoa dalili mpya kuhusu misimamo yake ya kichokozi katika ukanda huu, alisema kuwa Israel "imeweka wazi tena kuwa haitambui mamlaka ya nchi yoyote."

"Aidha, imeonyesha wazi kuwa ina uhusiano wa uhasama na karibu mataifa yote ya eneo hili," aliongeza.

Kurtulmus pia alisema kuwa tangu kamati hiyo ilipoanza vikao vyake, mojawapo ya malengo yake makuu limekuwa kuhakikisha kuwa "Uturuki isiyo na ugaidi itakuwa dhamana ya ukanda usio na ugaidi."

Pia alieleza matumaini yake si kwa Uturuki tu ambapo bunduki zitanyamazishwa, bali kwa ukanda mzima, “ambapo undugu utatawala, na tofauti za kikabila, kidini na kisiasa kati ya watu zitageuzwa kuwa njia za kuungana na kushirikiana.”

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us