UTURUKI
1 dk kusoma
Uturuki yakanusha madai kwamba Israel ililenga vikosi vyake nchini Syria
Wizara ya Ulinzi ya Uturuki imeonya kwamba kama Israel haitakomeshwa, mashambulio yake “yasiyokuwa na mipaka” yanaweza kuvuta eneo zima la Mashariki ya Kati kwenye maafa.
Uturuki yakanusha madai kwamba Israel ililenga vikosi vyake nchini Syria
Wizara ya Ulinzi ya Uturuki iliitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua haraka dhidi ya Israel. / / TRT World
11 Septemba 2025

Wizara ya Ulinzi ya Uturuki imekana ripoti ya kwamba Israel ililenga vifaa vya Vikosi vya Kijeshi vya Uturuki nchini Syria, ikisisitiza kuwa madai hayo “hayana ukweli wowote.”

Katika taarifa iliyotolewa Alhamisi, wizara hiyo ilielekeza macho yake kwenye shambulio la Israel nchini Qatar, ikisema hili ni ushahidi kwamba Tel Aviv imefanya ugaidi kuwa “sera ya taifa, inayochochea mizozo na kupinga amani.”

Ankara ilieleza kuwa shambulio hilo lilikuwa “ukiukaji mkubwa wa uhuru wa Qatar” na kutangaza: “Tunasimama kidete na Qatar dhidi ya shambulio hili.”

“Mashambulio yasiyo na mipaka”

Wizara hiyo ilitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua haraka, ikionya kuwa kama Israel haitakomeshwa, mashambulio yake yasiyokuwa na mipaka yanaweza kuleta maafa Mashariki ya Kati.

Shambulio la anga la Israel dhidi ya kikosi cha mazungumzo cha Hamas katika mji wa Doha limelaaniwa na kutajwa kama ukiukaji wa uhuru wa Qatar na sheria za kimataifa.

Shambulio hilo la Israel liliua wanachama watano wa Hamas pamoja na afisa mmoja wa usalama wa Qatar.

Hamas imethibitisha kuwa viongozi wake walinusurika katika shambulio hilo.

CHANZO:TRT World
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us