MICHEZO
1 dk kusoma
Fainali ya Klabu bingwa Ulaya nani kuibuka kidedea?
Uwanja wa Bayern Munich Allianz Arena ndiyo itakuwa sehemu ya maamuzi ya fainali ya klabu bingwa barani Ulaya wakati PSG ya Ufaransa itakapokabiliana na Inter Milan ya Italia.
Fainali ya Klabu bingwa Ulaya nani kuibuka kidedea?
Timu ya PSG. /Reuters
30 Mei 2025

Ni fursa nzuri bila shaka kwa PSG, licha ya kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya Ufaransa, Les Parisiens bado hawajafanikiwa kufikia kilele cha mafanikio yao Ulaya. Hii itakuwa nafasi yao ya kukamilisha hilo iwapo watapata ushindi katika mechi yao ya Jumamosi na kuweka historia kwenye klabu hiyo.

Kwenye fainali ya 2020 PSG ilifungwa 1-0 na Bayern Munich mjini Lisbon, Ureno wakiwa na kocha Thomas Tuchel. Luis Enrique anatarajia kufanya vizuri zaidi ya mtangulizi wake baada ya kuwatoa Arsenal katika hatua ya nusu fainali.

Timu ya PSG iliozoea ushindi wa Ligi Kuu ya Ufaransa ilishinda hatua zote mbili za nusu fainali na kutinga fainali kwa mara ya pili.

Wakati huohuo, Inter itakuwa inajaribu kujitoa kimasomaso baada ya msimu mbaya katika Ligi Kuu ya Italia. Vijana wa kocha Simone Inzaghi walishindwa katika ubingwa wa Ligi ya Serie A na Napoli.

Ni miaka 15 sasa tangu Nerazzurri waliposhinda taji la bara Ulaya. Kocha Jose Mourinho aliwapa ushindi wa mataji matatu 2010. Hata hivyo, Inter ilipambana katika fainali ya mwaka 2023, ingawa Manchester City walifanikiwa kuwapiku mabingwa hao mara 20 wa Ligi kuu ya Italia katika mechi iliyochezwa jijini Istanbul.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us