ULIMWENGU
1 DK KUSOMA
Mabaki yanayodhaniwa kuwa ya binadamu yamepatikana nyambizi ya Titan iliotoweka
Sehemu ndogo za vipande vya nyambizi zilizoharibika zimepatikana na kuondolewa mapema leo nchini Canada Mashariki, wakati operesheni ngumu ya kutafuta na kuopoa ikimalizika
Mabaki yanayodhaniwa kuwa ya binadamu yamepatikana nyambizi ya Titan iliotoweka
Mabaki ya binadamu yaaminika kupatikana katika vifusi vya nyambizi ya Titan iliotoweka | Picha: reuters / Others
29 Juni 2023

Wataalam wameopoa mabaki yanayodhaniwa kuwa ya binadamu kutoka kwa kile kilichobaki cha chombo cha Titan kilichozama wakati wa uchunguzi wa eneo kulikotokea ajali ya Titanic, na kusababisha vifo vya watu watano, kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Pwani ya Marekani.

"Wataalam wa afya wa Marekani watafanya uchunguzi rasmi wa mabaki yanayodhaniwa kuwa ya binadamu ambayo yameopolewa kwa uangalifu," taasisi hiyo ilisema.

Katika chombo hicho walikuwemo mtafiti wa Uingereza Hamish Harding, mtaalamu wa vyombo vya chini ya maji kutoka Ufaransa Paul-Henri Nargeolet, tajiri wa Kipakistani-Muingereza Shahzada Dawood na mwanae Suleman, pamoja na Stockton Rush, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya OceanGate Expeditions inayosimamia chombo hicho.

CHANZO:AFP
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us