ULIMWENGU
2 DK KUSOMA
Israeli yafanya shambulio kubwa la anga katika eneo la Gaza
Mashambulizi ya Israeli katika eneo la Gaza yameingia siku ya 258 na kuua Wapalestina 37,396, wengi wakiwa ni wanawake na watoto na kujeruhi wengine 85,523, huku wengine zaidi ya10,000 wakihofiwa kwenye vifusi.
Israeli yafanya shambulio kubwa la anga katika eneo la Gaza
Watoto wa Kipalestina wakicheza kwenye jua kali. / Picha: AA   / Others
20 Juni 2024

Mashambulizi ya anga ya Israeli katika eneo la Gaza yamesababisha vifo na majeruhi kwa Wapalestina, wengi wakiwa ni wanawake na watoto huku mashambulizi hayo yakiendelea.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Palestina la Wafa, wanawake wawili wameuwawa na wengine 12 kujeruhiwa katika shambulizi la angani katika nyumba moja kwenye kambi ya wakimbizi ya Nuseirat iliyoko katikati mwa Gaza.

Mizinga ya kijeshi ya Israeli ilishambulia maeneo ya kusini mwa kitongoji cha Zeitoun kusini mashariki mwa Mji wa Gaza, pamoja na maeneo ya mashariki ya kambi za wakimbizi za Maghazi ya kati na Bureij.

Matukio ya aina hiyo pia yaliripotiwa katika maeneo ya Rafah, eneo lililo kusini, huku mashambulizi ya silaha pia yakishuhudiwa.

Ikipuuzia azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kutaka kusitishwa mara moja kwa mapigano, Israeli imekabiliwa na shutuma za kimataifa huku kukiwa na kuendelea kwa mashambulizi ya kikatili dhidi ya Gaza tangu Oktoba mwaka jana.

Pata habari zaidi kupitia whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us