MICHEZO
2 DK KUSOMA
Tanzania yafuzu AFCON 2025
'Taifa Stars' inaungana na 'The Cranes' ya Uganda na 'Les Léopards' ya nchini DRC kama wawakilishi wa ukanda wa Afrika Mashariki katika michuano hiyo itakayotimua vumbi kuanzia Disemba 2025.
Tanzania yafuzu AFCON 2025
Simon Msuva wa 'Taifa Stars' aliweka kimiani bao katika dakika 61 na kuikatia Tanzania tiketi ya kushiriki michuano hiyo mikubwa barani Afrika./Picha:  @Tanfootball / Others
19 Novemba 2024

Bao pekee la dakika 61, lililotiwa kimiani na mshambuliaji anayeichezea Al-Talaba Sports Club ya nchini Iraq, Simon Msuva imeihakikishia 'Taifa Stars' tiketi ya kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), yatakayofanyika mwakani nchini Morocco.

Matokeo hayo, yanaifanya Tanzania kuungana na DRC na Uganda kama wawakilishi pekee kutoka ukanda wa Afrika Mashariki katika michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Kabla ya mchezo huo, ambao ulifanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, msimamo wa kundi H ulikuwa unaongozwa na DRC iliyokuwa na alama 12, ikifuatiwa na Guinea yenye 9, 'Taifa Stars' ikishika nafasi ya tatu kwa alama 7, huku Ethiopia ikiburuza mkia na alama1.

Hii itakuwa ni mara ya nne kwa Tanzania kushiriki michuano hiyo, ikiwa imefanya hivyo mwaka 1980, 2019 na 2023.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us